1 Corinthians 9:4-9

4 aJe, hatuna haki ya kula na kunywa? 5 bJe, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini, kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa?
Yaani Petro.
6 dAu ni mimi na Barnaba tu inatubidi kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu?

7 eNi askari yupi aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye shamba la mizabibu na asile matunda yake? Ni nani achungaye kundi na asipate maziwa yake. 8Je, nasema mambo haya katika mtazamo wa kibinadamu tu? Je, sheria haisemi vivyo hivyo? 9 fKwa maana imeandikwa katika Torati ya Musa: “Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka.” Je, Mungu hapa anahusika na ng’ombe?
Copyright information for SwhKC